Eswatini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Eswatini
Remove ads

Eswatini (jina rasmi: Ufalme wa Eswatini, pia Uswazi) ni nchi ndogo isiyo na pwani Kusini mwa Afrika. Imepakana na Afrika Kusini pande zote isipokuwa kaskazini mashariki inapopakana na Msumbiji. Mnamo 2023, Eswatini ilikuwa na idadi ya watu takriban milioni 1.2 na kuwa nchi ya 155 duniani kwa idadi ya watu. Miji mikuu ni Mbabane na Lobamba huku Mbabane ukiwa pia mji mkubwa nchini humo. Kiingereza na Kiswazi ndizo lugha rasmi.

Ukweli wa haraka Ufalme wa Eswatini Umbuso weSwatini (Kiswazi)Kingdom of Swaziland (Kiingereza), Miji mikuu ...
Remove ads

Historia

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Waswati walianzisha ufalme wao katikati ya karne ya 18 chini ya Ngwane III; mipaka ya sasa ilikubalika mwaka 1881.

Baada ya vita kati ya Waingereza na Makaburu, Swaziland ilukuwa nchi lindwa ya Uingereza tangu mwaka 1903 hadi 1967.

Chini ya mfalme Sobhuza II aliyetawala kwa muda mrefu sana (1921-1982), Swaziland ilipata uhuru tarehe 6 Septemba 1968.

Remove ads

Siasa

Eswatini inatawaliwa tangu mwaka 1986 na mfalme Mswati III. Mfalme anapingwa mara nyingi kwa sababu anatumia pesa nyingi kwa ajili yake binafsi ilhali wananchi ni maskini sana. Kwa muda mwingi wa uhuru wa nchi katiba imesimamishwa, na mfalme ametawala peke yake.

Watu

Thumb
Mwanamke kutoka Eswatini akicheza.

Wakazi wengi ni wa kabila la Waswati na kuongea lugha ya Kiswati ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza. Shuleni kinafundishwa pia Kireno.

Upande wa dini, 89.3% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, hasa Waprotestanti, lakini pia Wakatoliki (5%). Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% na Waislamu ni 1%.

Afya

Eswatini ni kati ya nchi duniani zilizoathiriwa zaidi na Ukimwi; umri wa wastani unafikia miaka 22 pekee kwa sababu ya vifo vingi (64%) vinavyotokana na ugonjwa huo uliopata 26% ya watu wazima wote.

Tanbihi

Tazama pia

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads