Eugenius wa Karthago
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Eugenius wa Karthago (alifariki 13 Julai 505) alikuwa Mkristo aliyechaguliwa kwa kauli moja kuwa askofu wa mji huo mwaka 480 baada ya Deogratias wa Karthago (aliyefariki 456).

Ilimbidi atetee imani sahihi kwa kupambane na Uario, ulioungwa mkono na mfalme wa Wavandali. Alifaulu kuwavuta baadhi yao katika Kanisa Katoliki na kwa sababu hiyo alifukuzwa akaishi uhamishoni katika jangwa la Libia [1].
Halafu aliruhusiwa kurudi, lakini miaka minane baadaye akafukuzwa tena ahamie Vienne, karibu na Albi (leo nchini Ufaransa). Huko alijenga monasteri aliposhika maisha ya toba hadi kifo chake[2].
Kutokana na imani na maadili yake, tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.
Remove ads
Maandishi
- Expositio Fidei Catholicae
- Apologeticus pro Fide
- Altercatio cum Arianis.[4]
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads