Libya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Libya ni nchi ya Afrika ya Kaskazini kwenye Bahari ya Mediteranea, inayopakana na Misri, Sudan, Niger, Chad, Algeria na Tunisia. Eneo kubwa la nchi (90%) ni sehemu ya jangwa la Sahara. Chini yake kuna akiba kubwa ya petroli, ambayo ndiyo utajiri wa nchi. Miji mikuu ni Tripoli, Benghazi na Misratah.
Jamhuri ya Libya دولة ليبيا (Dawlat Lībiyā) | |
---|---|
Wimbo wa taifa: Libya, Libya, Libya
| |
Mji mkuu na mkubwa | Tripoli |
Lugha rasmi | Kiarabu |
Kabila | 92% Waarabu, 5% Waberber, 3% wengine |
Dini | 96.6% Uislamu (rasmi), 2.7% Ukristo, 0.7% nyingine |
• Mwenyekiti wa Baraza la Rais | Mohamed al-Menfi |
• Waziri Mkuu | Abdul Hamid Dbeibeh |
Eneo | |
• Jumla | km2 1,759,541 |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2024 | ▲ 7,361,263 |
• Msongamano | 4.184/km2 |
PLT (PPP) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $183.39 bilioni [1] |
• Kwa kila mtu | ▲ $26,928 [1] |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $48.22 bilioni [1] (ya 93) |
• Kwa kila mtu | ▲ $6,987 [1] |
HDI (2022) | ▲ 0.746 (ya 92) juu |
Sarafu | Dinar ya Libya (LYD) |
Majira ya saa | UTCUTC+2 |
Upande wa magari | Kulia |
Msimbo wa simu | +218 |
Jina la kikoa | .ly |

Historia
Wakazi asili walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki.
Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo ukaenea.
Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi.
Katika karne ya 7 Waarabu waliingiza Uislamu na utamaduni wao.
Mwaka 1551 Waturuki walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala hadi karne ya 20.
Nchi ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941 ilipotekwa na Waingereza ambao, baada ya Vita vikuu vya pili kwisha, waliacha nchi mwaka 1951 mikononi mwa mfalme mwenyeji, Idris I, aliyekuwa amepinga ukoloni tangu mwaka 1920 (Vita vya Libya dhidi ya Italia).
Kisha kumpindua mfalme huyo, Muammar al-Gaddafi alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011 kwa mkono wa N.A.T.O.
Baada ya hapo wananchi wanazidi kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mwaka 2020 kulikuwa na makubaliano ya kusimamisha vita na kuunda serikali ya pamoja ili kuandaa uchaguzi mkuu.
Watu
Wakazi wa Libya ni hasa mchanganyiko wa Waberberi, Waarabu na Waturuki (74%), mbali na Waberberi (25%) ambao ndio wakazi asilia, lakini wengi wao wameanza kutumia lugha ya Kiarabu pia. Kuna pia wahamiaji kutoka nchi za jirani, za kandokando ya Bahari ya Kati na kutoka Bara Hindi.
Wakazi wameongezeka tangu mwaka 1970 kutoka milioni 2.5 hadi kuwa karibu milioni 7 mwaka 2022. Nusu ya wakazi wote ni vijana chini ya umri wa miaka 16. Sehemu kubwa kabisa (80%) huishi sehemu za pwani.
Lugha kuu ni Kiarabu pamoja na lugha kadhaa za Kiberberi. Ndizo:
- Kinafusi (wasemaji 101.000)
- Kighadames (wasemaji 42.000)
- Kitamascheq (Tuareg; wasemaji 17.000)
Upande wa dini, unatawala Uislamu (97%). Wakristo ni zaidi ya 100,000, wakiwemo hasa Wakopti (60,000) na Wakatoliki (40,000).
Tazama pia
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.