Gaudioso wa Napoli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gaudioso wa Napoli (jina kamili kwa Kilatini: Septimius Celius Gaudiosus; pia: Sanctus Gaudiosus Africanus, yaani Mtakatifu Gaudioso Mwafrika; 385 - 455) alikuwa askofu wa Abitine, karibu na Karthago, leo nchini Tunisia.
Mwaka 439 alikimbia Afrika Kaskazini wakati wa dhuluma za Genseriki, mfalme wa Wavandali, dhidi ya Wakatoliki akahamia Napoli pamoja na askofu wa Karthago, Quodvultdeus, na wengineo.
Alifariki kitakatifu monasterini. Inasadikika kwamba ndiye aliyeingiza huko kanuni ya Augustino wa Hippo.[1][2]
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads