Henri Walpole
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Henri Walpole, S.J. (Docking, Norfolk, 24 Januari, 1558 – York, 7 Aprili 1595) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza.

Baada ya kushuhudia kifodini cha Edmundi Campion (1581) alishika imani hadi kupewa upadrisho huko Paris, Ufaransa (1588), alijiunga pia na Wajesuiti.
Alipokuwa tena Uingereza kufanya utume kinyume cha sheria za nchi wakati wa malkia Elisabeti I alikamatwa na kufungwa, aliteswa kikatili na hatimaye alinyongwa na kuraruliwa vipandevipande[1] pamoja na padri mwenzake Aleksanda Rawlins.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929 na mtakatifu na Papa Paulo VI mwaka 1976.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 7 Aprili[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads