Mkoa wa Manyara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa wa Manyara ni mojawapo ya mikoa ya Tanzania ulioko kaskazini mwa Tanzania, wenye makao makuu mjini Babati. Unapakana na Mkoa wa Arusha upande wa kaskazini, Mkoa wa Kilimanjaro kaskazini-mashariki, Mkoa wa Tanga mashariki, Mkoa wa Dodoma kusini, na Mkoa wa Singida upande wa magharibi. Mandhari ya Manyara yanajumuisha sehemu ya Bonde la Ufa pamoja na Ziwa Manyara, ambalo limetoa jina kwa mkoa huu. Mkoa huu unajulikana kwa shughuli za kilimo, ufugaji, na utalii, hasa kupitia Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara na vivutio vya kiutamaduni vinavyotokana na jamii za asili kama Wamasai na Waarusha.


Mkoa wa Manyara umetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa na eneo la km² 46,359.
Remove ads
Wakazi
Jumla ya wakazi mkoani ilikuwa 1,892,502 katika sensa ya mwaka 2022 [1].
Idadi hiyo imepatikana katika wilaya 7 zifuatazo (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022): Babati Vijijini (375,200), Babati Mjini (129,572), Hanang (367,391), Mbulu Vijijini (238,272), Mbulu Mjini (138.593), Simanjiro (291,169) na Kiteto (352,305).
Sensa zinaonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi. Pia ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi.
Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaqw, Wamasai, Wambugwe, Wagorowa na Wabarbaig wakijihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku.
Remove ads
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi 7 yafuatayo:
- Babati Mjini : mbunge ni Pauline Gekuli (CCM)
- Babati Vijijini : mbunge ni Jitu Vrajilal Soni (CCM)
- Hanang’ : mbunge ni Samwel Hhayuma (CCM)
- Kiteto : mbunge ni Emmanuel Papiani (CCM)
- Mbulu Mjini : mbunge ni Zacharia Paulo Issaay (CCM)
- Mbulu Vijijini : mbunge ni Flatei Massay (CCM)
- Simanjiro : mbunge ni James Kinyasi Ole Millya (CCM)
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads