Joakima wa Vedruna

From Wikipedia, the free encyclopedia

Joakima wa Vedruna
Remove ads

Joakima wa Vedruna (jina kamili kwa Kikatalunyaː Joaquima de Vedruna Vidal de Mas; Vic, Barcelona, Hispania, 17 Aprili 1783 - Sevilla, 28 Agosti 1854) alikuwa sista mwanzilishi wa shirika la Masista Wakarmeli wa Upendo ambalo ndani ya Kanisa Katoliki linahudumia vijana, wagonjwa na wazee waliosahaulika. Kwa sasa lina masista 2,000 hivi duniani kote[1].

Thumb
Mt. Joakima mwaka 1903.

Kabla ya hapo aliishi katika ndoa akazaa watoto tisa aliowalea Kikristo sana [2], lakini baada ya kufiwa mumewe alianzisha shirika hilo kwa kuvumilia aina nyingi za matatizo hadi alipofariki dunia kwa kipindupindu[3].

Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 19 Mei 1940, halafu Papa Yohane XXIII alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Aprili 1959.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads