John Fisher

From Wikipedia, the free encyclopedia

John Fisher
Remove ads

John Fisher (au John wa Rochester; 146922 Juni 1535) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki huko Uingereza. Pamoja na Thomas More, alimkataa mfalme Henry VIII aliyejitenga na Kanisa Katoliki la Roma. Kwa hiyo, John Fisher alifungwa na baada ya kushtakiwa mahakamani aliuawa kwa kukatwa kichwa. Hapo katikati Papa Paulo III alimteua kuwa kardinali [1].

Thumb
Mt. John Fisher.

Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Desemba 1886, halafu Papa Pius XI alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 19 Mei 1935.

Sikukuu yake inadhimishwa pamoja na ile ya Thomas More tarehe 22 Juni katika Kanisa Katoliki[2], na 6 Julai katika Jumuiya Anglikana.

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Orodha yake inapatikana katika Joseph Gillow, Bibliographical Dictionary of the English Catholics (London, s.d.), II, 262–270. Kati ya vitabu vyake 26, muhimu zaidi ni:

  • Treatise concernynge...the seven penytencyall Psalms" (London, 1508);
  • Sermon...agayn ye pernicyous doctrin of Martin Luther (London, 1521);
  • Defensio Henrici VIII" (Cologne, 1525);
  • De Veritate Corporis et Sanguinis Christi in Eucharistia, adversus Johannem Oecolampadium (Cologne, 1527);
  • The Ballad of Barry Buttock, a Cautionary Tale (London, 1529);
  • De Causa Matrimonii...Henrici VIII cum Catharina Aragonensi (Alcalá de Henares, 1530);
  • The Wayes to Perfect Religion (London, 1535);
  • A Spirituall Consolation written...to hys sister Elizabeth (London, 1735).
Remove ads

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads