Thomas More

From Wikipedia, the free encyclopedia

Thomas More
Remove ads

Thomas More (7 Februari 14786 Julai 1535) alikuwa mwanasheria kutoka Uingereza.

Thumb
Thomas More

Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Desemba 1886, halafu Papa Pius XI alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 19 Mei 1935.

Sikukuu yake inaadhimishwa pamoja na ile ya John Fisher tarehe 22 Juni kufuatana na kalenda rasmi ya Kanisa Katoliki[1], na 6 Julai katika Jumuiya Anglikana.

Maisha

Thomas More alizaliwa katika mji wa London tarehe 7 Februari mwaka 1478.

Alisoma katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza, akaoa na kupata watoto wanne.

Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mahakama wa Uingereza.

Aliandika vitabu kadhaa kuhusu mambo ya kiserikali, na vingine vya kutetea imani ya Kanisa Katoliki.

Pamoja na Mt. John Fisher alishindana na Mfalme Henri VIII kuhusu suala la kuivunja ndoa ya huyo mfalme. Kwa amri ya Henri, wote wawili waliopinga kuvunjwa kwa ndoa yake walifungwa gerezani na kuuawa kwa kukatwa kichwa, kwanza John Fisher tarehe 22 Juni, halafu Thomas More tarehe 6 Julai, mwaka 1535[2].

Remove ads

Sala yake

Bwana mwema, utujalie neema ya kuyafanyia kazi yale tunayokuomba.

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi: “CW” inarejelea Yale Edition of the Complete Works of St. Thomas More (New Haven and London 1963–1997)

Yaliyotolewa akiwa hai (mwaka)

  • A Merry Jest (c. 1516) (CW 1)
  • Utopia (1516) (CW 4)
  • Latin Poems (1518, 1520) (CW 3, Pt.2)
  • Letter to Brixius (1520) (CW 3, Pt. 2, App C)
  • Responsio ad Lutherum (1523) (CW 5)
  • A Dialogue Concerning Heresies (1529, 1530) (CW 6)
  • Supplication of Souls (1529) (CW 7)
  • Letter Against Frith (1532) (CW 7)
  • The Confutation of Tyndale's Answer (1532, 1533) (CW 8)
  • Apology (1533) (CW 9)
  • Debellation of Salem and Bizance (1533) (CW 10)
  • The Answer to a Poisoned Book (1533) (CW 11)

Yaliyotolewa baada ya kifo chake(mwaka wa utungaji)

  • The History of King Richard III (c. 1513–1518) (CW 2 & 15)
  • The Four Last Things (c. 1522) (CW 1)
  • A Dialogue of Comfort Against Tribulation (1534) (CW 12)
  • Treatise Upon the Passion (1534) (CW 13)
  • Treatise on the Blessed Body (1535) (CW 13)
  • Instructions and Prayers (1535) (CW 13)
  • De Tristitia Christi (1535) (CW 14)

Tafsiri

  • Translations of Lucian (many dates 1506–1534) (CW 3, Pt.1)
  • The Life of Pico della Mirandola (c. 1510) (CW 1)
Remove ads

Tanbihi

Loading content...

Marejeo

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads