Jose Vaz

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jose Vaz
Remove ads

Jose Vaz, CO, (kwa Kikonkani: Zuze Vaz; kwa Kireno: José Vaz; kwa Kitamil: புனித யோசப் வாஸ், Punidha Yosap Vaz; kwa Kisinhala: ශාන්ත ජුසේ වාස් මුනිතුමා, ශ්‍රී ලංකාවේ අපොස්තුළුවරයා, Santha Juse Vaz Munithuma, Sri Lankawe Aposthuluvaraya; Benaulim, Goa, India, 21 Aprili 1651  Kandy, Sri Lanka, 16 Januari 1711) alikuwa padri wa Oratorio ya Mt. Filipo Neri, mmisionari nchini Sri Lanka.

Thumb
Mt. Jose Vaz.

Vaz alifika huko wakati kisiwa hicho kimetekwa na Waholanzi, ambao walitaka kulazimisha Ukalvini uwe dini rasmi . Bila kujali dhuluma yao, Jose aliizunguka nchi yote akiwapatia Ekaristi na sakramenti nyingine Wakatoliki waliobaki baada ya Wareno kufukuzwa. Kwa namna hiyo Vaz alidumisha Kanisa Katoliki nchini, hata akaitwa mtume wa Ceylon [1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 21 Januari 1995, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 14 Januari 2015.[2]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Vyanzo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads