Juan Diego

From Wikipedia, the free encyclopedia

Juan Diego
Remove ads

Juan Diego Cuauhtlatoatzin (yaani Yohane Diego Anayesema-kama-tai, 1474 hivi - 30 Mei 1548) ni kati ya Wakristo wa kwanza wa Mexico.

Thumb
Picha ya Juan Diego Cuauhtlatoatzin.
Thumb
Kadiri ya mapokeo, picha hii ya Bikira Maria wa Guadalupe ilipatikana kwa muujiza katika koti la Juan Diego, kwenye kilima cha Tepeyac karibu na Mexico City tarehe 12 Desemba 1531.

Mlei huyo ni maarufu hasa kwa kusadikiwa kwamba alitokewa na Bikira Maria akiwa na sura ya chotara.

Mwenye imani safi sana, kwa unyenyekevu na ari yake alifanya pajengwe patakatifu kwa heshima ya Bikira Maria wa Guadalupe katika mlima Tepeyac karibu na Mji wa Mexiko, alipokuwa ametokewa na ambapo hatimaye alifariki dunia kitakatifu[1].

Njozi hiyo ilifuatwa haraka sana na wongofu wa Waindio wenzake milioni 8 wa nchi hiyo ambao walibatizwa kati ya mwaka 1532 na 1538.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mwaka 1990, halafu 2002 akamtangaza mtakatifu, wa kwanza kati ya wakazi asili ya Amerika.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 9 Desemba[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads