Kalemie
mji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kalemie ni mji wa J.K. Kongo uliopo kando ya ziwa Tanganyika upande wa magharibi kwa kimo cha mita 785 juu ya UB pale ambako mto Lukuga unapotoka ziwani. Mwaka 2005 Kalemie ilikuwa na wakazi 147,000. Kuna bandari muhimu yenye mawasiliano kwa meli na Kigoma (Tanzania) na Bujumbura (Burundi).

Kalemie iliundwa kama kituo cha kijeshi tarehe 30 Desemba 1891 upande wa kusini wa chanzo cha mto Lukuga ziwani na kapteni Mbelgiji Jacques de Dixmude kwa jina la Albertville kwa heshima ya mfalme mtarajiwa Albert wa Ubelgiji. Mji ulikua baada ya kufika kwa reli ya Kongo.
Kalemie ni mwisho wa reli; mipango ya kale ya ukoloni ilikuwa kwamba njia ya reli kutoka Atlantiki ingeishia hapa itakayoounganishwa kwa feri na bandari ya Kigoma penye chanzo cha reli ya Tanganyika kwenda Dar es Salaam. Kutokana na miaka mingi ya fujo reli ya Kongo haikukamilishwa kamwe: haifiki hadi Atlantiki lakini kuna njia ya reli kuanzia Kalemie hadi jimbo la Katanga.
Kuna viwanda vya nguo na saruji.
Mwaka 2005 mji uliathiriwa na tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads