Kanoaldi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kanoaldi (pia: Chagnoald, Cagnoald, Canoeld, Cagnou, Canoaldus; karne ya 6 - 633 hivi) alikuwa askofu wa 6 wa Laon (Ufaransa) baada ya kuwa mmonaki huko Luxeuil chini ya Kolumbani (594)[1] .
Huyo alipofukuzwa na mfalme Theuderiki II (610), Kanoaldi alikwenda naye kuinjilisha eneo la Bregenz, kando ya ziwa la Konstanz (Ujerumani) [2], halafu aliongozana naye hadi Roma.
Hatimaye aliweza kuongoza jimbo lake hadi alipofariki dunia[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu kama ndugu zake Faro na Fara[4].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Septemba[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads