Kaunti ya Mandera
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kaunti ya Mandera ni mojawapo ya Kaunti 47 za Kenya iliyopo kaskazini mashariki mwa nchi. Inapakana na Ethiopia upande wa kaskazini, Somalia upande wa mashariki, na Kaunti ya Wajir upande wa kusini-magharibi. Kulingana na sensa ya 2019 kaunti hii ilikuwa na wakaazi 867,457 ikiwa kaunti ya 24 kwa idadi ya watu na eneo la km2 25,939.8 na kuwa kaunti ya 6 kwa ukubwa wa ardhi.[1].Mji mkubwa na makao makuu ni mji wa Mandera. Inajulikana kwa misukosuko ya usalama na uhamiaji kutoka Somalia
Remove ads
Jiografia
Kaunti hii ina mbuga ya pekee ya Kaskazini Mashariki ya Malka Mari na hifadhi ya kibinafsi ya Chacnabole. Ina vilima vinavyotandaa kutoka El Wak hadi Uhabeshi ingawa kiasi kikubwa cha ardhi yake ni nchi tambarare.
Kuna kanda mbili za ikolojia, kavu na nusu kavu. 95% ya kaunti ni nusu kavu na huwa na vichaka vyenye miiba katika sehemu za chini za vilima[2].
Utawala
Kaunti ya Mandera imegawanywa katika maeneo yafuatayo[3]:
Remove ads
Demografia
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]
- Mandera West 98,300
- Banisa 152,598
- Kutulo 72,394
- Lafey 83,457
- Mandera Central 157,220
- Mandera East 159,638
- Mandera North 143,850
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads