Kilifi

Mji nchini Kenya From Wikipedia, the free encyclopedia

Kilifi
Remove ads

Kilifi ni mji kwenye pwani ya kusini ya Kenya uliopo kati ya Mombasa na Malindi. Iko kando ya kihori cha Kilifi ("Kilifi Creek") kinachoishia katika Bahari Hindi.

Ukweli wa haraka Nchi, Kaunti ...
Thumb
Kilifi, Kenya
Thumb
Madau kwenye kihori cha Kilifi Creek

Mji ni makao makuu ya Kaunti ya Kilifi.

Wakati wa sensa ya mwaka 2009 Kilifi ilikuwa na wakazi 122,899 [1].

Kilifi imekuwa kitovu kimojawapo cha utalii nchini Kenya hasa kutokana na fuko zake za kupendeza na Bofa Beach ni marufuku hasa. Mdomo mpana wa kihori unapendwa na wenye jahazi za burudani, hivyo kuna jahazi nyingi zinazolala hapa.

Remove ads

Historia

Kulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale.

Maghofu ya kihistoria ya Mnarani yako kando ya mji wa Kilifi. Mabaki yanayoonekana ni misikiti miwili pamoja na makaburi yaliyokuwa sehemu ya mji wa Waswahili uliokuwa kituo cha biashara. Msikiti mkubwa ulianzishwa mnamo mwaka 1425; mji uliangamizwa wakati wa mashambulio ya Waoromo katika karne ya 17.

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads