Kiyiddish
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kiyiddish (kwa lugha ya wenyewe: יידיש; kwa Kiingereza: Yiddish) ni lugha inayotumiwa na Wayahudi.

Ilikuwa lugha kuu ya Wayahudi wengi duniani, hasa katika Ulaya ya Kati na Ulaya ya Mashariki hadi maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya. Tangu maangamizi hayo idadi ya wasemaji imepungua sana, leo kuna takriban wasemaji 600,000 duniani.
Ni tofauti na Kiebrania ambayo ni lugha ya kidini ya Wayahudi na lugha rasmi katika nchi ya Israeli, lakini huandikwa kwa herufi za Kiebrania.
Asili yake ni Kijerumani cha zamani pamoja na Kiebrania. Ilianzishwa na Wayahudi wa Ujerumani takribani miaka 1,000 iliyopita. Wakati wa mateso dhidi yao katika Vita za Misalaba, Wayahudi wengi walianza kuhamia Polandi ambako jumuiya kubwa ya Wayahudi duniani ilikuwa. Katika jamii za Wayahudi wa Polandi (iliyojumuisha maeneo ya Polandi, Lithuania, Ukraine na Belarus za leo) Kijerumani cha wahamiaji Wayahudi kutoka magharibi kilienea kikawa lugha yao ya pamoja; waliita "lugha ya Kiyahudi", kwa matamshi yao: "yiddish".
Asilimia kubwa ya msamiati ni Kijerumani cha Kale; kuna makadirio ya kwamba takriban asilimia 70 ya maneno ni kutoka Kijerumani, asilimia 20 kutoka Kiebrania na asilimia 10 kutoka lugha za Kislavoni, yaani mazingira ya wasemaji wa Kiyiddish[1].
Katika karne ya 19 maeneo yenye wasemaji wa Kiyiddish yaliwekwa chini ya utawala wa Milki ya Urusi na kutokana na mateso dhidi ya Wayahudi milioni kadhaa walianza kuhamia Marekani walipoendelea kutumia Kiyiddish. Mnamo mwaka 1939, kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, idadi ya wasemaji ilikadiriwa kuwa mnamo milioni 11. Nusu yao waliuawa katia maangamizi makuu na wengi waliobaki walihamia Israeli, Marekani au nchi nyingine, ambako wengi wao walijifunza lugha ya nchi na kwa njia hiyo utamaduni wa Kiyiddish ilipotea katika familia.
Leo hii wasemaji wako hasa katika Marekani, hasa katika jumuiya ya Wahasidi, na nchini Israeli.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads