Kolmani wa Dromore

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kolmani wa Dromore (pia: Mocholmóc; alifariki karne ya 6) alikuwa abati[1][2][3] wa monasteri aliyoianzisha huko Dromore[4], halafu pia askofu wa mji huo[5] katika kisiwa cha Ireland. Alijitahidi sana kueneza imani ya Kikristo katika eneo la Down[6].

Pengine anachanganywa na Kolmani mwingine aliyekuwa askofu katika Visiwa vya Orkney huko Uskoti na kufariki mwaka 1010 hivi[7][8].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Papa Leo XIII alithibitisha heshima hiyo tarehe 19 Juni 1902[9].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Juni[10].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads