Kua

Ndege wakubwa kiasi wa jenasi Coua, familia Cuculidae From Wikipedia, the free encyclopedia

Kua
Remove ads

Kua (kutoka Kimalagasy: koa) ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Coua katika nusufamilia Phaenicophaeinae ya familia Cuculidae. Pengine wanaainishwa katika nusufamilia yao Couinae pamoja na kekeo-ardhi wa Asia (Carpococcyx). Jenasi pekee ya Bara la Afrika inayoainishwa katika Phaenicophaeinae ni Ceuthmochares (ukiki). Kua ni ndege wa Madagaska wanaofanana na kekeo. Wana mkia mrefu na miguu mirefu. Kidole cha tatu cha miguu yao kinaweza kukabili mbele au nyuma. Rangi kuu ni kijivu na/au buluu na wana ngozi tupu kuzunguka macho yenye rangi buluu. Kua hula mbegu, matunda madogo, wadudu na wanyama wadogo kama mijusi na vigeugeu. Kinyume na kekeo, kua hulijenga tago lao lenyewe. Jike huyataga mayai meupe 1-3 (2 mara nyingi zaidi).

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Spishi za kabla ya historia

  • Coua berthae, Kua wa Bertha (Bertha's Coua) – Mwisho wa Quaternary
  • Coua primaeva, Kua wa Kale (Ancient Coua) – Mwisho wa Quaternary

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads