Leonardo wa Portomaurizio

From Wikipedia, the free encyclopedia

Leonardo wa Portomaurizio
Remove ads

Leonardo wa Portomaurizio (Porto Maurizio, leo Imperia, 20 Desemba 1676 - Roma 26 Novemba 1751) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki kutoka Italia.

Thumb
Leonardo akiwa amevaa kanzu yake ya Kifransisko.

Ndiye tunda bora la Kirekebisho cha utawa wa Ndugu Wadogo kilichoanzia mjini Roma karne XVII.

Ni maarufu hasa kwa mahubiri yake ya wiki nzima (wiki za uamsho) aliyoyaendesha karibu mfululizo kati ya waamini wa Kanisa Katoliki kotekote nchini Italia na katika kisiwa cha Corsica (leo nchini Ufaransa), akisisitiza hasa ibada kwa mateso ya Yesu kwa kupitia vituo 14 vya Njia ya Msalaba.

Akiwa amejaa upendo kwa wokovu wa watu, aliendesha wiki hizo mara 343, akiongozana kwa kawaida na mapadri 4 na bradha 1. Baada ya wiki mbili za mahubiri kulikuwa na wiki moja ya maungamo.

Katika miaka 44 aliokoa watu wengi ajabu, na kuinua hali ya kiroho ya mapadri wanajimbo na watawa, pamoja na kuandika vitabu vya kuhamasisha maisha ya kiroho[1].

Ndiye mwenezaji mkuu wa Njia ya Msalaba, ibada iliyoanza kustawi katika karne XV ikiwa na vituo 7 hadi 37, mpaka ile ya 14 ilipopewa rehema ya pekee (1686) na hivyo kuenea popote.

Papa Pius VI alimtangaza mwenye heri, halafu Papa Pius IX akamtangaza mtakatifu tarehe 29 Juni 1867.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Remove ads

Sala yake

Yesu wangu, kwa haki tu na kwa shukrani napaswa kujitoa kabisa kwako, baada ya wewe kujitoa kabisa kwangu...

Wewe umetakasa hisi zangu zote; fanya ziwe zako, zisifurahie tena kilicho kinyume cha sheria yako ya Kimungu.

Umetakasa kumbukumbu yangu; iwe inakukumbuka mfululizo.

Umetakasa utashi wangu; usigeuke kamwe kupenda chochote kuliko wewe.

Basi, kutoka dhati ya moyo wangu nakutolea kama sadaka kamili ya kudumu, kadiri ninavyoweza, mwili wangu na roho yangu, hisi zangu na vipawa vyangu, nilichonacho na jinsi nilivyo.

Ee moto wa Kimungu, choma, Ee Upendo wa Mwenyezi, choma na kuteketeza yale yote yasiyo yako ndani mwangu! Amina.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads