Ludoviko IX
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ludoviko IX (maarufu kama Mtakatifu Alois; Poissy, karibu na Paris, Ufaransa, 25 Aprili 1214 – Tunis, Tunisia, 25 Agosti 1270) alikuwa mfalme wa Ufaransa tangu 1226 hadi kifo chake.



Anahesabiwa kuwa mtawala bora wa Kikristo kwa jinsi alivyoishi kwa imani wakati wa amani na wakati wa vita alivyovipiga kwa nguvu zote ili kutetea Wakristo waliodhulumiwa, alivyojali ibada, msalaba, taji la miba na kaburi la Bwana, alivyotenda haki katika kuongoza nchi, alivyoheshimu ndoa yake na kulea vizuri watoto wake 11, alivyohudumia wananchi, hasa maskini na wagonjwa, na alivyovumilia matatizo yaliyompata [1].
Alifariki dunia kwa tauni aliyoambukizwa kwa kuwahudumia askari zake wakati wa vita vya msalaba.
Ni mfalme pekee wa nchi hiyo kutangazwa mtakatifu (na Papa Boniface VIII, 1297).
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads