Waindio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Waindio au Wahindi wekundu ni watu wanaotokana moja kwa moja na waliokuwa wenyeji wa Amerika kabla ya bara hilo kufikiwa na Christopher Columbus kutoka Ulaya (1492).

Asili

Utafiti uliofanywa kwa muda mrefu na kwa njia mbalimbali umekadiria kwamba mababu wao walioenea katika Amerika yote wakitokea Asia kaskazini mashariki miaka 14,500 BK.
Inadhaniwa kwamba hao mababu waliishi muda mrefu na kuzaliana bila mawasiliano na binadamu wengine, labda katika eneo ambalo leo limefunikwa na maji kwenye mlangobahari wa Bering. Inakadiriwa DNA yao ilitokana na ile ya Waasia mashariki (2/3) na Waeurasia (1/3).
Baada ya kuingia bara hilo, ambalo ni la mwisho kukaliwa na watu (tukiacha Antaktiki), kwa karne chache walienea hadi kusini kabisa, kwenye Chile na Argentina ya leo. Katika kusambaa kwao, lugha na utamaduni vilizidi kutofautiana.
Remove ads
Hali ya sasa
Idadi yao inaweza kuwa milioni 60, wengi wao wakiishi Meksiko, Peru, Bolivia na Guatemala.
Tanbihi
Vyanzo
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads