Mark Twain

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mark Twain
Remove ads

Mark Twain lilikuwa jina la kisanii la Samuel Langhorne Clemens (30 Novemba 1835 - 21 Aprili 1910) aliyekuwa mwandishi nchini Marekani.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Amekufa ...
Mark Twain (1909)
Remove ads

Maisha

Alizaliwa katika mji wa Florida kwenye jimbo la Missouri akaendelea kuwa mwandishi wa magazeti na baadaye nahodha wa meli ya mto Missisippi.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani ilizuia usafiri wa mtoni akaenda magharibi alipojaribu kuchimba dhahabu akaanza tena kuandika kwenye gazeti.

Mwaka 1863 alianza kuandika kwa jina la kuchaguliwa "Mark Twain". Jina hilo lilitokana na lugha ya mabaharia likimaanisha "alama mbili" kwenye uzi wa kupima kina cha maji chini ya meli ni kina kinachohitajika kwa safari. Kwa jina hilo alitoa hadithi za kichekesho zilizopendwa na watu akajenga sifa yake.

Akatumwa na magazeti kwa safari akiendelea kutoa taarifa za kichekesho juu ya safari zake.

Baadaye alitoa pia riwaya. Kati ya vitabu vyake ambavyo hutazamwa kama bora ni Huckleberry Finn ambayo ni hadithi ya kijana Mzungu anayemsaidia mtumwa mwenye asili ya Afrika kupata uhuru wake katika majimbo ya kusini ya Marekani.

Remove ads

Maandiko

  • The Adventures of Tom Sawyer (1876)
  • The Prince and the Pauper (1882)
  • Adventures of Huckleberry Finn (1884)
  • A Connecticut Yankee in King Arthur's Court (1889)

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads