Martino wa Tours
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Martino wa Tours (Savaria, Panonia, leo Hungaria 316 - Candes-Saint-Martin, Gaul, leo Ufaransa 397) alikuwa mmonaki, halafu askofu (kuanzia 371 hadi kifo chake).





Kisha kuzaliwa na Wapagani, aliitwa jeshini sehemu za Ufaransa. Huko, akiwa bado mkatekumeni, alimfunika kwa joho lake Kristo aliyetwaa sura ya fukara.
Baada ya kubatizwa, aliacha jeshi na kuishi kitawa huko Ligugé katika monasteri aliyoianzisha mwenyewe, akiwa chini ya uongozi wa Hilari wa Poitiers.
Hatimaye alipewa daraja takatifu ya upadri akachaguliwa kuwa askofu wa Tours, akawa mfano wa Mchungaji mwema, akianzisha monasteri nyingine na parokia vijijini, akifundisha na kupatanisha waklero na kuinjilisha wakulima hadi mwisho kabisa wa maisha yake [1].
Alipokaribia kifo, walimuomba asiondoke, naye akasali hivi: "Ee Bwana, nikihitajiwa bado na watu wako, sikatai uchovu wa kazi: utakalo lifanyike!"
Maisha yake yaliandikwa na Sulpicius Severus yakawa kielelezo cha vitabu juu ya watakatifu.
Sifa yake ilienea haraka hivi kwamba aliheshimiwa kama mtakatifu ingawa hakuwa mfiadini kama kawaida ya wakati ule. Hadi leo anaheshimiwa hivyo na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri n.k.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 11 Novemba[2], ila kwa Waorthodoksi tarehe 11 Oktoba.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads