Masimo wa Torino
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Masimo wa Torino (labda 380 hivi – 420 hivi) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki na mwanateolojia kutoka Italia Kaskazini.

Mwanafunzi wa watakatifu Eusebi wa Vercelli na Ambrosi wa Milano, alipata kuwa askofu wa Torino, Italia, kwa miaka 30 hivi, tena ndiye wa kwanza kujulikana katika ya maaskofu wake.
Kwa maneno yake ya kibaba alivuta umati wa Wapagani kwenye imani ya Kikristo akawaongoza kwa mafundisho ya Kimungu kwenye tuzo ya wokovu[1].
Alitunga hotuba mia kadhaa [2] na vitabu sita.
Ingawa maisha yake hayajulikani sana, huyo babu wa Kanisa anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads