Mkoa wa Singida
mkoa wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania: mkoa huo upo kanda ya kati, ukipakana na mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Arusha upande wa kaskazini, Manyara na Dodoma upande wa mashariki, Iringa na Mbeya upande wa kusini, hatimaye Tabora upande wa magharibi. Eneo lake ni la km2 49,340. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa wakazi 2,008,058 [1] kutoka 1,370,637 wa mwaka 2012[2]. Makao makuu ya mkoa yako Singida.

Msimbo wa posta ni 43000.
Remove ads
Wilaya na wakazi
Kuna wilaya saba za Iramba, Manyoni, Singida Vijijini na Singida Mjini, Ikungi, Itigi na Mkalama.
Wakazi wa wilaya za Singida mjini na vijijini ni hasa Wanyaturu. Walio wengi Iramba ndio Wanyiramba, Wagogo wakiwa wengi huko Manyoni. Pia kati ya wenyeji kuna Wanyisanzu na makabila mengine madogo. Makabila hayo wanaishi kwa amani na upendo.
Lugha kuu ni Kiswahili, lakini pia kila kabila wanaongea yao.
Remove ads
Uchumi
Singida ni kati ya maeneo maskini zaidi ya Tanzania. Uchumi wake unategemwa hasa ufugaji: idadi ya ng'ombe hukadiriwa kuwa takribani milioni 1.4, mbali na punda, kondoo, kuku n.k. Masoko hayako karibu na barabara si nzuri.
Kilimo si kizuri kwa sababu ya uchache wa mvua. Ukame huleta njaa. Singida ni kati ya mikoa inayotegemea misaada ya chakula. Kati ya mazao yapo ya chakula na ya biashara. Mazao yanayolimwa mkoani hapo ni mtama, alizeti, vitunguu, uwele, viazi, mahindi, karanga, maharagwe n.k.
Pamoja na kuwa mkoa wa Singida umekuwa ukikumbwa na njaa kwa sababu ya ukame, na hata pale mvua inaponyesha ni duni sana, una shughuli mbalimbali ambazo zinaingiza kipato kwa watu wa mkoa huo.
Ikiwa kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea mpaka sasa imekuwa madini ya dhahabu yakigunduliwa katika sehemu mbalimbali mkoani Singida japo kumekuwa aidha hakufanyiwi uchunguzi wa kina kuhakiki kiwango cha hifadhi ya madini iliyopo katika eneo husika au huwa kiwako kilichopo ni kidogo, hivyo kutokuvutia wawekezaji wakubwa katika maeneo hayo. Kati ya madini ambayo yamewahi kugunduliwa katika mkoa wa Singida ni dhahabu ambayo imewahi kugunduliwa huko Londoni na Iruma wilayani Manyoni.
Mkoani Singida kuna mapori mengi ya akiba ambayo yamejaa wanyama wa aina nyingi ambao kama mapori hayo yatafanywa kuwa hifadhi kamili za taifa yatasaidia sana kuvutia utalii na kuufanya mkoa wa Singida uongeze pato lake na kupunguza umaskini miongoni mwa wanajamii kwani utatoa ajira kwa jamii inayozunguka hifadhi hizo.
Remove ads
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Singida Mjini : mbunge ni Mussa Sima (CCM)
- Singida Kaskazini : mbunge ni Lazaro Nyalandu (CCM)
- Iramba Mashariki : mbunge ni Joseph Allan Kiula (CCM)
- Iramba Magharibi : mbunge ni Mwigulu Nchemba (CCM)
- Manyoni Magharibi : mbunge ni Yahya Omari Masare (CCM)
- Manyoni Mashariki : mbunge ni Daniel Edward Mtuka (CCM)
- Singida Mashariki : mbunge ni Tundu Lissu (Chadema)
- Singida Magharibi : mbunge ni Elibariki Emmanuel Kingu (CCM)
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads