Modoaldi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Modoaldi (Akwitania, leo nchini Ufaransa, 584/590 - Trier, leo nchini Ujerumani, 12 Mei 645/648) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 620 hivi[1].

Kabla ya kuchaguliwa alifanya kazi ikulu bila kupendezwa na maadili mabovu ya huko[2].
Baadaye alijenga na kupamba makanisa na kuanzisha monasteri mbalimbali na jumuia za mabikira kwa kusaidiana na dada yake Severa, ambaye hatimaye alizikwa karibu naye [3] [4].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads