Msaada wa Wakristo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Msaada wa Wakristo
Remove ads

Msaada wa Wakristo (kwa Kilatini: Auxilium Christianorum) ni sifa mojawapo ya Bikira Maria katika Kanisa Katoliki.

Thumb
Maria Msaada wa Wakristo alivyochorwa na Tommaso Lorenzone, kwa agizo la Yohane Bosco, 1867 hivi, Torino.
Thumb
Patakatifu pa Maria Ausiliatrice huko Torino, palipoanzishwa na padri Yohane Bosco. Juu ya kuba kuna sanamu ya Maria Msaada wa Wakristo.

Yohane Krisostomo alikuwa wa kwanza kutumia jina hilo mwaka 345.

Baadaye, Ukristo ulipoatharishwa na uenezi wa Waislamu, waumini walimkimbilia Maria kwa jina hilo ili kupata msaada wa sala zake. Hasa mwaka 1571, Waturuki walipokaribia kuteka Ulaya, Papa Pius V aliombea jeshi la Kikristo kwa kuagiza sala ya Rozari hadi ushindi ulipopatikana katika mapigano ya Lepanto.

Yohane Bosco ndiye aliyeeneza zaidi heshima hiyo.

Mtaguso wa pili wa Vatikano, katika hati juu ya Kanisa (61, 62), ulitaja jina hilo ukieleza umama wa Maria[1].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Mei[2].

Remove ads

Katika sanaa

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads