Papa Pius V
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Pius V, O.P. (17 Januari 1504 – 1 Mei 1572) alikuwa Papa kuanzia tarehe 7/17 Januari 1566 hadi kifo chake[1]. Alitokea Alessandria, Italia[2].

Alimfuata Papa Pius IV akafuatwa na Papa Gregori XIII.
Umuhimu wake katika historia ya Kanisa ni kwamba ndiye alishughulikia kwa moyo wa ibada na bidii ya kitume utekelezaji wa Mtaguso wa Trento kwa ajili ya urekebisho wa Kikatoliki, ukiwa pamoja na vitabu vya liturujia, katekesi na maadili, ili kueneza imani [3].
Anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Maisha
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Antonio Ghislieri.
Baadaye alijiunga na shirika la Wahubiri.
Kama kardinali, Ghislieri alijulikana kwa kutanguliza usahihi wa imani kuliko vyeo vya watu, akihukumu maaskofu wanane wa Ufaransa kwa uzushi. Vilevile alipinga upendeleo wowote kwa ndugu wa ukoo, akimkemea mtangulizi wake Papa Pius IV alipotaka kumfanya kardinali mtoto wa miaka 13 kwa kuwa ni ndugu yake, tena alipotaka kumsaidia ndugu mwingine kwa fedha za hazina ya Papa.
Kwa hati "Regnans in Excelsis" ya mwaka 1570, Pius V alitenga na Kanisa Katoliki malkia Elizabeth I wa Uingereza kwa uzushi na kwa kudhulumu Wakatoliki wa nchi yake.
Mwaka 1571 aliunganisha nchi za Kikatoliki katika "Liga Sancta" ambayo katika mapigano ya Lepanto, ingawa ilizidiwa na Dola la Osmani kwa idadi ya wanajeshi, ilifaulu kulizuia lisiteke Ulaya nzima. Pius V aliona ushindi huo umetokana na maombezi ya Bikira Maria aliyekuwa ameombwa sana kwa rozari siku zile, akaanzisha sikukuu ya Bibi Yetu wa Ushindi.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads