Nabii Shemaya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nabii Shemaya (kwa Kiebrania שְׁמַעְיָה, Šəmaʿyā, maana yake: "YHWH amesikia"; alikuwa nabii nchini Israeli katika karne ya 10 KK.


Chanzo kikuu cha historia yake ni Kitabu cha Kwanza cha Wafalme (12:22-24) pamoja na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati (11:2-4; 12:5-7).
Kadiri ya vitabu hivyo, alimzuia mfalme Rehoboamu asipigane vita na Yeroboamu I ili kujirudishia mamlaka juu ya makabila ya kaskazini yaliyoasi[1].
Pia alimtabiria Rehoboamu adhabu ya Mungu kumpitia farao Shishak wa Misri kwa makosa yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Mengineyo
Katika Biblia ya Kiebrania kuna watu wengine kumi na saba wenye jina hilohilo, tena inataja Kitabu cha nabii Shemaya kama chanzo cha habari kadhaa, lakini kitabu hicho kimepotea hata leo.
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads