New Delhi

From Wikipedia, the free encyclopedia

New Delhi
Remove ads

New Delhi (yaani Delhi Mpya; kwa Kihindi: |नई दिल्ली, kwa Kiurdu: نئی دلی) ni mji mkuu wa Uhindi na kitovu cha jiji kubwa la Delhi. Pamoja na Delhi yote kuna wakazi zaidi ya milioni kumi.

Ukweli wa haraka Nchi ...
Thumb
"India Gate" mjini New Delhi.
Thumb
Boma Jekundu la Delhi ni jengo mashuhuri lililojengwa kwa Shah Jahan.
Thumb
Majengo ya serikali katika Delhi Mpya yalijengwa na Waingereza.
Remove ads

Jiografia

Iko kaskazini mwa nchi kwenye kingo za mto Yamuna katika tambarare ya bonde la Ganga. Mji huo uko m 216 juu ya UB kwa wastani.

Historia

Delhi ina historia ndefu sana iliyoanza mnamo mwaka 1200 KK. Iliharibiwa mara nyingi na kujengwa upya na kubadilisha jina pamoja na wakazi na watawala wake. Katika karne zilizopita ilikuwa mji mkuu wa Dola la Moghul na tangu mwaka 1911 wa Uhindi wa Kiingereza.

Delhi Mpya ilianzishwa baada ya azimio la George V, mfalme wa Uingereza na Kaisari wa Uhindi, la kuhamisha mji mkuu kutoka Kolkata kwenda Delhi. Mji mpya ulijengwa kando ya Delhi ya Kale na kukabidhiwa mwaka 1931. Ulisanifiwa na wasanifu Waingereza Edwin Lutyens (1869-1944) na Herbert Baker (1862-1946).

Tangu mwaka 1947 New Delhi ni mji mkuu wa Uhindi huru.

Remove ads

Tazama pia

  • Orodha ya wakuu wa majimbo ya India

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu New Delhi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads