Papa Adrian VI

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Adrian VI
Remove ads

Papa Adrian VI (2 Machi 145914 Septemba 1523) alikuwa Papa kuanzia tarehe 9 Januari/31 Agosti 1522 hadi kifo chake[1]. Alitokea Utrecht, Uholanzi[2]. Alikuwa Mholanzi pekee kuwa Papa, na alikuwa Papa wa mwisho asiye Mwitalia hadi Papa Yohane Paulo II kutoka Polandi alipochaguliwa miaka 455 baadaye [3].

Thumb
Papa Adrian VI alivyochorwa na Jan van Scorel.
Thumb
Papa Adrian VI alivyochorwa mwaka 1568.
Thumb
Nyumba ya kuzaliwa ya Papa Adrian na shairi linaloandamana. Maelezo ya mchongo wa 'Wanaume na Wanawake Maarufu wa Uholanzi'.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Adriaan Florensz, hivyo hakubadili jina la ubatizo alipochaguliwa kuwa Papa, tofauti na watangulizi na waandamizi karibu wote wa milenia ya pili.

Alimfuata Papa Leo X akafuatwa na Papa Klementi VII.

Remove ads

Maisha

Mzaliwa wa Utrecht (leo nchini Uholanzi), Adriano alisoma katika chuo kikuu cha Leuven akawa mwalimu wa teolojia na makamu wa gombera huko.

Mwaka 1507 akawa mlezi wa atakayekuwa kaisari Karolo V wa Dola Takatifu la Roma (Ujerumani), ambaye baadaye alimtumia katika nafasi muhimu.

Mwaka 1516, Adriano akawa askofu wa Tortosa, Hispania, halafu hakimu mkuu wa imani wa falme za Aragona na Castilya.

Mwaka 1517 Papa Leo X alimteua kuwa kardinali na mwaka 1522 akachaguliwa kuwa mwandamizi wake.

Adriano alianza upapa wake katikati ya matatizo makubwa ajabu, uenezi wa Walutheri upande wa kaskazini, na wa Waturuki Waosmani upande wa mashariki.

Kuhusu mafundisho ya imani, alikataa kukubaliana na Walutheri, akidai Martin Luther ahukumiwe kuwa mzushi. Hata hivyo, alijitahidi kurekebisha Kanisa Katoliki. Juhudi zake zilishindikana kwa sababu ya kupingwa na makardinali na maaskofu wengi waliofuata anasa kadiri ya mtindo wa Renaissance, tena kwa sababu aliwahi kufa.

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads