Papa Klementi VII
Papa wa Kanisa Katoliki kutoka 1523 hadi 1534 From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Klementi VII (kwa Kilatini: Clemens VII; kwa Kiitalia: Clemente VII; 26 Mei 1478 – 25 Septemba 1534) alikuwa Papa na mtawala wa Dola la Papa kuanzia tarehe 19/26 Novemba 1523 hadi kifo chake[1]. Alitokea Firenze, Italia[2][3][4].

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giulio di Giuliano de' Medici. Akitajwa kuwa "papa aliyekuwa na bahati mbaya zaidi," utawala wake ulikuwa na mfululizo wa migogoro ya kisiasa, kijeshi, na kidini mingi ikiwa imeanza kabla ya enzi yake iliyokuwa na athari kubwa kwa Ukristo na siasa za dunia.[5]
Alishiriki katika vita kati ya Kaizari Karoli V wa Ujerumani-Hispania na Mfalme Fransisko I wa Ufaransa, akisimama kwanza na kaizari, baadaye na mfalme. Mwaka 1527 alikamatwa baada ya Roma kutekwa na jeshi la kaizari. Katika amani ya mwaka 1529, wakati wa mashambulio ya Waturuki dhidi ya Vienna, alirudishwa uhuru wake pamoja na utawala juu ya Dola la Papa katika Italia ya Kati, akikubali kipaumbele cha kaizari juu ya Italia ya Kaskazini. Mwaka 1530 alimwekwa Karolo V wakfu kama kaizari wa Dola Takatifu la Kiroma.
Katika miaka 1529 hadi 1534 Klementi VII aliwasiliana mara kwa mara na Mfalme Henry VIII wa Uingereza aliyetaka kibali cha Papa kutengana na mke wake wa kwanza. Papa alipokataa, mfalme aliagiza bunge lake kutangaza uhuru wa Kanisa la Uingereza; hatimaye Papa alimtenga mfalme Henry na Kanisa Katoliki kwenye mwaka 1534.
Alimfuata Papa Adrian VI akafuatwa na Papa Paulo III.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
