Papa Agatho
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Agatho alikuwa Papa kuanzia tarehe 27 Juni 678 hadi kifo chake tarehe 10 Januari 681[1]. Alitokea Sicilia, Italia[2][3].

Alitetea imani sahihi dhidi ya wazushi waliosema Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu na aliendesha sinodi kadhaa ili kuimarisha umoja wa Kanisa.
Inasemekana kwamba alikuwa na umri wa zaidi ya miaka mia moja alipochaguliwa kuwa Papa, na alikuwa ametunza hazina ya Kanisa kwa miaka mingi[4].
Wakati wa Upapa wake ulifanyika Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli (680-681) uliofundisha rasmi kwamba Yesu, chini ya utashi wake wa Kimungu, alikuwa na utashi wa kibinadamu pia[5].
Alimfuata Papa Donus akafuatwa na Papa Leo II.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu yake tarehe 10 Januari[6], lakini Waorthodoksi tarehe 20 Februari.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads