Papa Dionysius
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Dionysius alikuwa Papa kuanzia tarehe 22 Julai 259 hadi kifo chake tarehe 26 Desemba 269[1].

Alimfuata Papa Sisto II akafuatwa na Papa Felisi I.
Alifanya kazi kubwa ya kupanga upya Kanisa baada ya dhuluma ya kaizari Valerian iliyoacha Roma bila askofu kwa karibu mwaka mzima[2]. Mtu aliyejaa maadili mema, alitumia uhuru uliopatikana upya chini ya kaisari Gallienus na kudumu miaka 40 [3], akifariji kwa barua zake na uwepo wake ndugu wenye huzuni, akikomboa wafungwa katika mateso yao na kuwafundisha misingi ya imani wasioijua [4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Maandishi yake
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads