Papa Sixtus II
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Sixtus II alikuwa Papa kuanzia tarehe 30 Agosti 257 hadi kifodini chake tarehe 6 Agosti 258[1]. Alitokea Ugiriki[2].

Alimfuata Papa Stefano I akafuatwa na Papa Dionysius.
Alirudisha umoja na makanisa ya Mashariki na Afrika Kaskazini uliowahi kuhatarishwa na misimamo tofauti kuhusu ubatizo uliotolewa na waliojitenga na Kanisa Katoliki.
Alikamatwa akihubiria ndugu wa imani juu ya sheria za Mungu wakati wa adhimisho la ekaristi[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini pamoja na mashemasi wake sita: Januari, Vinsenti, Magnus, Stefano, mbali ya Agapito na Felisisimi waliouawa siku hiyohiyo sehemu nyingine chini ya kaisari Valeriani[4]. Katika Kanuni ya Kirumi anatajwa pamoja na shemasi wake wa saba, Laurenti, aliyeuawa siku tatu baadaye.
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads