Papa Celestino V
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Celestino V, O.S.B. (1215 – 19 Mei 1296) alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Julai/29 Agosti 1294 hadi 13 Desemba 1294[1]. Alitokea Molise, Italia[2].

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Pietro Angelerio wa Morrone. Baada yake hakuna tena Papa aliyejichagulia jina la Celestino.
Alimfuata Papa Nikolasi IV baada ya miaka miwili ya pengo[3], akichaguliwa kutokana na umri wake mkubwa na sifa ya utakatifu na utendaji miujiza [4].
Ni maarufu kwa kuwa mwaka uleule alijiuzulu[5] kwa kujitambua hawezi Upapa [6] ili arudi kuishi maisha ya upwekeni kama mmonaki (mwaka 1244 alikuwa ameanzisha shirika la Waselestini, tawi la Wabenedikto)[7]. Lakini Papa Bonifasi VIII aliyemfuata alimfunga akafuta karibu maamuzi yake yote.
Alitangazwa na Papa Klementi V kuwa mtakatifu tarehe 5 Mei 1313[8].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads