Papa Silverio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Silverio alikuwa Papa kuanzia tarehe 8 Juni 536 hadi mwaka 537[1]. Alitokea Frosinone, Italia[2].

Alimfuata Papa Agapeto I akafuatwa na Papa Vigilio.
Alizaliwa na Papa Hormisdas katika ndoa yake kabla ya kupata upadrisho.
Aliondoshwa madarakani mnamo mwezi Machi 537 kwa nguvu ya Theodora, mke wa Justiniani I, Kaisari wa Bizanti.
Huyo malkia alimpendelea shemasi Vigilio akitarajia ataunga mkono njama zake za kutetea uzushi wa Eutike.
Kumbe Silverio alikataa pia ombi la Theodora la kumrudisha madarakani Antimo kama Patriarki wa Konstantinopoli aliyekuwa ameondolewa na Papa Agapeto I kwa uzushi huohuo [3].
Basi, Silverio alifungwa na kupelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Palmarola ambapo alijiuzulu tarehe 11 Novemba 537 akafariki kwa tabu nyingi na njaa tarehe 2 Desemba 537.
Angalau tangu karne ya 11 ameheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads