Papa Agapeto I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Agapeto I alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Mei 535 hadi kifo chake tarehe 22 Aprili 536[1]. Alitokea Roma, Italia[2].
Alimfuata Papa Yohane II akafuatwa na Papa Silverio.
Alidai kwa nguvu Papa achaguliwe na waklero wa Roma bila kuingiliwa na yeyote na hadhi ya Kanisa iheshimiwe popote pale.
Mfalme wa Wagoti Teodoto alimtuma Konstantinopoli kwa kaisari Justiniani I, na huko alisimama imara dhidi ya Waario, pia alimwondoa madarakani Anthimus I, askofu mkuu wa Trabzon (Uturuki) aliyehamishimiwa na serikali kuwa Patriarki wa Konstantinopoli, kutokana na mafunzo yake yaliyoangaliwa na Kanisa Katoliki kuwa ya uzushi. Badala yake alimweka wakfu Mena wa Konstantinopoli akafariki huko [3].
Zimetufikia barua zake nne [4]
Muda si mrefu baada ya kifo chake alianza kuheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads