Papa Silvester I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Silvester I alikuwa Papa kuanzia tarehe 31 Januari 314 hadi kifo chake tarehe 31 Desemba 335[1].

Alimfuata Papa Miltiades akafuatwa na Papa Marko.
Mtoto wa Rufinus, mkazi wa Roma, hatuna habari nyingi za maisha yake. Ila ni kwamba aliongoza kwa busara Kanisa Katoliki kwa muda mrefu mara baada ya Kaisari Konstantino Mkuu kulipatia uhuru wa dini na kulijengea maabadi mengi, makubwa tena mazuri.
Wakati wa utawala wake ulifanyika mtaguso mkuu wa kwanza (Nisea, leo nchini Uturuki, 325) uliomshangilia Kristo kama Mwana wa Mungu. Yeye hakuhudhuria, ila alituma wajumbe wawili akathibitisha maamuzi yaliyofikiwa.
Alizikwa katika katakombu la Prisila [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads