Papa Stefano I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Stefano I alikuwa Papa kuanzia tarehe 12 Machi 254 hadi kifodini chake tarehe 2 Agosti 257[1][2]. Alitokea Roma, Italia, ingawa aliweza kuwa na asili ya Ugiriki.

Alimfuata Papa Lucius I akafuatwa na Papa Sisto II.
Alifundisha kwamba waliobatizwa na madhehebu yaliyojitenga na Kanisa Katoliki wameungana na Kristo moja kwa moja, hivyo hawahitaji wala hawatakiwi kubatizwa tena[3], tofauti na walivyodai baadhi ya maaskofu, hasa wa Afrika Kaskazini. Baadaye msimamo wake ulienea kote katika Kanisa la Kilatini.
Inasimuliwa kwamba aliuawa na maaskari wa Kaisari Valerian wakati wa Misa[4] .
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads