Papa Lucius I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Lucius I alikuwa Papa kuanzia Juni au Julai 253 hadi kifo chake tarehe 5 Machi 254[1]. Alitokea Roma, Italia.

Alimfuata Papa Kornelio akafuatwa na Papa Stefano I.
Kwa imani yake kwa Kristo, mara baada ya kuwekwa wakfu alipelekwa uhamishoni, lakini aliwahi kurudishwa, akatoa ushahidi wake kwa kukabili kwa upole na busara matatizo ya wakati wake[2][3].
Sipriani wa Carthago alimsifu [4] kwa kukataa msimamo mkali wa wafuasi wa Novasyano dhidi ya waliowahi kuasi ili kuokoa uhai wao.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe ya kifo chake[5][6].
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads