Pierre Borie
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Pierre-Rose-Ursule Dumoulin-Borie (20 Februari 1808 – 24 Novemba 1838) alikuwa padri Mkatoliki wa Ufaransa aliyefanya kazi kama mmisionari wa Paris Foreign Missions Society huko Vietnam hadi alipokatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Minh Mang [1].



Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 27 Mei 1900, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 19 Juni 1988 katika kundi la Wafiadini wa Vietnam.
Remove ads
Maisha
Kisha kujiunga na seminari ya Servières mwaka 1824, alipata upadrisho huko Bayeux tarehe 21 Novemba 1830 akatumwa ng'ambo, akifikia Macao tarehe 18 Julai 1831.
Akikwepa vizuizi vya serikali dhidi ya umisionari, alifaulu kufikia Saigon na kujiunga na misheni ya Tonkin Kusini (Vietnam).
Bila kujali dhuluma ya serikali, alidumu kutekeleza majukumu yake ya kichungaji katika eneo alilokabidhiwa mpaka alipokamatwa mwaka 1838.
Akiwa gerezani, alipata taarifa ya kuwa ameteuliwa kuwa askofu tangu tarehe 30 Januari 1836.
Muda mfupi baadaye, tarehe 24 Novemba 1838, aliambiwa amehukumiwa adhabu ya kifo akauawa siku hiyohiyo pamoja na mapadri wenzake Petro Vo Bang Khoa (1790 - 1838) na Vinsenti Nguyen The Diem (1761 - 1838).
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads