Prokoro mwinjilisti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Prokoro mwinjilisti ni Myahudi wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Jumuiya Anglikana tarehe 28 Julai pamoja na wenzake Nikanori, Timone, Parmena na Nikola wa Antiokia[1][2].
Remove ads
Katika Biblia
Alikuwa mmojawapo kati ya wanaume saba wa lugha ya Kigiriki katika Kanisa mama la Yerusalemu ambao, wakiwa wamejaa Roho Mtakatifu na hekima, walichaguliwa na waumini wenzao wakawekewa mikono na Mitume wa Yesu ili kushughulikia kwa niaba yao huduma za fukara (Mdo 6)[3].
Katika mapokeo
Mapokeo ya baadaye yanasimulia kwamba alikuwa ndugu wa Stefano, alifuatana na Mtume Petro au Mtume Yohane aliyemfanya askofu wa Nikomedia katika Uturuki wa leo.
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads