Proto na Yasinto

From Wikipedia, the free encyclopedia

Proto na Yasinto
Remove ads

Proto na Yasinto (walifariki 257/259) ni kati ya Wakristo wa Misri waliofia imani yao huko Roma, Italia, katika dhuluma ya kaisari Valerian.

Thumb
Kifodini cha Wat. Proto na Yasinto, mchoro mdogo wa karne ya 14.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Papa Damaso I aliwasifu kwa mashairi na kutoa masalia yao ardhini. Karne 15 baadaye vimepatikana tena huko kaburi la Yasinto zima kabisa na mifupa yake imeunguzwa kwa moto kutokana na jinsi alivyouawa [1].

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 11 Septemba[2] au 24 Desemba.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads