Reykjavík
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Reykjavík (tamka: Reykyavik) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Isilandi wenye wakazi 113,387. Ni mji mkuu wa dunia ulio kaskazini zaidi kushinda miji mikuu ya nchi zote huru.

Jiografia
Iko kwenye pwani ya kusini ya Isilandi mwambaoni mwa hori ya Faxaflói.
Reykjavik inafaidi kukaa mahali pa kukutana kwa mabamba ya gandunia ya Ulaya na Amerika ya Kaskazini. Magma ya koti ya dunia iko karibu na uso wa nchi na inasababisha maji kwenye ardhi kuwa ya moto. Maji ya moto hayo hutumiwa kwa kupasha moto nyumba za watu na mabanda ya bustani. Nishati inapatika kwa urahisi kiasi kwamba katika mazingira ya barafu kuna hata mavuno ya ndizi kwenye bustani hizo zinazopata moto kwa maji yale ya kutoka chini ya ardhi.
Remove ads
Historia
Inaaminiwa ya kwamba Reykjavík ilikuwa mahali pa makazi ya kwanza ya watu walioanza kufika kisiwani mnamo mwaka 870. Mwanzilishi wa makazi hayo alikuwa Mnorwei Ingólfur Arnarson. Hadi karne ya 18 hapakuwa na mji bali rundiko la nyumba za wakulima tu.
Mji wenyewe ulianzishwa huko mwaka 1786 kama kituo cha biashara ukaendelea kukua. Leo hii ni mji wa kisasa kabisa na kitovu cha uchumi, utamaduni na siasa vya Isilandi.
Remove ads
Hali ya hewa

Kutokana na mahali pake karibu na ncha ya kaskazini Reykjavik haioni kabisa giza la usiku wakati wa miezi Mei - Julai lakini wakati wa Novemba - Januari kuna saa nne tu za mwanga wakati wa mchana.
Trafiki
Kuna huduma za mabasi ya mjini, ya mkoa na ya eneo la Strætó. Bandari za feri zipo Reykjavik na bandari ya Seydisfjordur, mashariki mwa Isilandi. Uwanja wa ndege uko Keflavik karibu na Reykjavik.
Picha za Reykjavik
- Perlan
- Kanisa Kuu la Reykjavík
- Uwanja wa Lækjartorg mjini
- Barabara mjini Reykjavík
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Reykjavík kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads