Rikitrude
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rikitrude (pia: Rictrude, Rictrudis, Richtrudis, Richrudis; 612 - 12 Mei 688) alikuwa mwanamke wa ukoo maarufu wa Ufaransa Kusini Magharibi ambaye tangu ujanani aliongozwa kiroho na Amando akaolewa na Adalbati I akaishi naye maisha maadilifu sana[1][2] .

Baada ya mumewe kuuawa, kwa ushauri wa Amando alijiunga na monasteri ya Marchiennes aliyokuwa ameianzisha, akawa abesi wake[3] na kuongoza vizuri sana mabikira waliowekwa wakfu huko[4].
Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, sawa na mume wake na watoto wao wote wanne, Klotsinda, Adalsinda, Eusebia wa Douai na Morandi.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads