Ruaruke

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Ruaruke ni kata ya Wilaya ya Kibiti katika Mkoa wa Pwani, Tanzania, yenye postikodi namba 61812.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 11,283 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,229 [2] walioishi humo.

Wakazi ni hasa Wandengereko na Wamyagatwa (Wazaramo) pia kuna makabila mengine ya wahamiaji kama vile Wasukuma, Wamang'ati na Waha.

Dini kuu ni Uislamu na Ukristo.

Wakazi wa Ruaruke wanajishughulisha zaidi na kilimo pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mazao yanayolimwa ni ya biashara na chakula. Mazao ya biashara ni korosho, ufuta na mihogo. Mazao ya chakula ni mpunga na mahindi; mihogo hutumika kama zao la chakula na la biashara.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads