Saint Martin

From Wikipedia, the free encyclopedia

Saint Martin
Remove ads

Saint Martin (jina rasmi la Kifaransa ni Collectivité de Saint-Martin) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa linalopatikana kaskazini mwa kisiwa chenye jina hilo, ambacho thuluthi ya kusini ni mwanachama wa Ufalme wa Nchi za Chini, mbali ya visiwa vingine vidogo.

Thumb
Kisiwa cha Saint Martin
Thumb
Saint-Martin na sehemu ya bahari ya Karibi iliyo chini yake.
Thumb
Ramani ya kisiwa ikionyesha Saint-Martin ya Kifaransa (kaskazini) na Sint Maarten ya Kiholanzi (kusini).

Ukubwa wa eneo ni kilometa mraba 53.2.

Makao makuu yako Marigot.

Idadi ya wakazi ni 35,107 (mnamo Januari 2014).

Kabla ya mwaka 2007 ilikuwa chini ya Guadeloupe.[1][2]

Mkataba wa Lisbon unaweka wazi kuwa Saint-Martin ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.[3]

Wakazi wanaongea hasa Kiingereza na Krioli yake, mbali ya Kifaransa ambacho ndicho lugha rasmi.

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads