Sherehe kuu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Sherehe kuu 12 (kwa Kigiriki: Δωδεκάορτον, Dodekaorton) za Makanisa ya Kiorthodoksi, tukiacha Pasaka iliyo sikukuu ya sikukuu zote, zinawaadhimisha Yesu Kristo (8) pamoja na Bikira Maria (4).[1]

Ni hizi zifuatazo:

  1. 21 Septemba [O.S. 8 Septemba], Kuzaliwa kwa Mama wa Mungu
  2. 27 Septemba [O.S. 14 Septemba], Kutukuka kwa Msalaba
  3. 4 Desemba [O.S. 21 Novemba], Mama wa Mungu kutolewa hekaluni
  4. 7 Januari [O.S. 25 Desemba], Kuzaliwa kwa Kristo/Krismasi
  5. 19 Januari [O.S. 6 Januari], Ubatizo wa KristoTheofania, inayoitwa pia Epifania
  6. 15 Februari [O.S. 2 Februari], Yesu kutolewa hekaluni
  7. 7 Aprili [O.S. 25 Machi], Kupashwa Habari Maria
  8. Jumapili kabla ya Pasaka — Kuingia Yerusalemu Jumapili ya Matawi au ya Mitende au ya Maua
  9. Siku arubaini baada ya Pasaka — Yesu Kristo Kupaa Mbinguni
  10. Siku hamsini baada ya Pasaka — Pentekoste
  11. 19 Agosti [O.S. 6 Agosti], Yesu Kugeuka Sura
  12. 28 Agosti [O.S. 15 Agosti], Kulala kwa Mama wa Mungu

Mbali ya hizo, Waorthodoksi wana sherehe nyingine tano zinaazohesabiwa kuwa kuu: Tohara ya Kristo 14 January [O.S. 1 January], Kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji 7 Julai [O.S. 24 Juni], Watakatifu Petro na Paulo 12 July [O.S. 29 June], Kukatwa Kichwa kwa Yohane Mbatizaji 11 Septemba [O.S. 29 Agosti], na Ulinzi wa Mama wa Mungu 14 Oktoba [O.S. 1 Oktoba].[2]

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads