Kugeuka sura

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kugeuka sura
Remove ads

Yesu kugeuka sura ni sikukuu ya liturujia ya Ukristo inayoadhimisha fumbo la maisha ya Yesu linalosimuliwa katika Agano Jipya[1], hususan katika Injili Ndugu (Math 17:1–9, Mk 9:2-8, Lk 9:28–36) na katika 2 Pet 1:16–18[1].

Thumb
Mozaiki ya Kugeuka sura, Monasteri ya Mt. Katerina, Mlima Sinai, Misri.
Thumb
Mchoro mdogo wa Kugeuka sura katika Injili ya Marko, 1300.
Thumb
Mchoro wa karne ya 12.
Thumb
Kugeuka sura kadiri ya Lodovico Carracci, 1594: wanaoonekana pamoja na Yesu ni Eliya, Musa na Mitume wa Yesu watatu.
Thumb
Mchoro wa Alexandr Ivanov, 1824.
Thumb
Kanisa la Kugeuka Sura juu ya Mlima Tabor, Israeli, unaohesabiwa na wengi kuwa mahali pa tukio.

Humo tunasoma kwamba Yesu Kristo aliongozana na wanafunzi wake watatu, Mtume Petro, Yakobo Mkubwa na mdogo wake Mtume Yohane, hadi mlima kwa lengo la kusali faraghani.

Huko usiku alianza kung'aa akatokewa na Musa na Eliya waliozungumza naye kuhusu kufariki kwake Yerusalemu.

Kubwa zaidi, Mungu Baba alimshuhudia kuwa Mwana wake mpenzi akawahimiza wanafunzi hao kumsikiliza.[1]

Hivyo Wakristo wanaona tukio hilo kama dhihirisho la Mwana pekee wa Mungu, mpendwa wa Baba wa milele, lililokusudiwa kuonyesha hadi miisho ya dunia kwamba hali duni ya binadamu aliyoitwaa imekombolewa kwa neema na kwamba jinsi ilivyoumbwa kwa mfano wa Mungu, sasa imeumbwa upya katika Kristo baada ya uharibifu uliosababishwa na Adamu [2].

Tukio linaheshimiwa hasa na Ukristo wa Mashariki na wamonaki wanaoliona mwaliko wa kutazama utukufu wa Mungu uliofichama katika malimwengu, kumbe kwa sala unadhihirika kwa macho ya imani.

Fumbo hilo linaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu tarehe 6 Agosti[3]. Pia linazingatiwa katika Rozari kama tendo la nne la mwanga.

Remove ads

Picha

Ukristo wa Mashariki

Ukristo wa Magharibi

Makanisa na monasteri

Remove ads

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads